Hivi karibuni suala la walemavu wa ngozi (albino) limechukua sura mpya kufuatia mauaji ya kikatili wanayofanyiwa. Ulemavu wa ngozi ni tatizo linalorithiwa kutokana na ukosefu wa pigment katika
...Click here to read more
Hivi karibuni suala la walemavu wa ngozi (albino) limechukua sura mpya kufuatia mauaji ya kikatili wanayofanyiwa. Ulemavu wa ngozi ni tatizo linalorithiwa kutokana na ukosefu wa pigment katika nywele, ngozi na macho. Ni tatizo linalowapata watu bila kujali kabila wala jinsia. Huko Marekani na Ulaya inakadiriwa kwamba mtu mmoja kati ya 20,000 huwa na dalili za ulemavu wa ngozi, wakati hapa kwetu Tanzania takwimu zinaonyesha kuwa mmoja kati ya watu 4,000 ana dalili za ulemavu huo. Kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) Tanzania ina walemavu wa ngozi takriban 170,000.
Tangu mwaka 2007, Tanzania imekuwa ikishuhudia mauaji ya kikatili ya albino ambayo yanahusishwa na ukataji wa viungo mbalimbali vya miili yao. Wengi wao wamepoteza maisha huku wengi wameachwa wakiwa hawana baadhi ya viungo vyao vya mwili baada ya kukatwa na kunyofolewa kikatili. Inasadikika kwamba mpaka sasa karibu albino 43 wameuwawa na viungo vyao kunyofolewa.
Kati ya sababu zinazotajwa kupelekea unyama huu ni imani za kishirikina kuwa baadhi ya viungo vya mwili wa albino vina uwezo wa kuleta utajiri. Serikali ya Tanzania imefanya jitihada nyingi kukabiliana na tatizo hili ikiwa ni pamoja na kusitisha shughuli za waganga wa jadi ambao inasemekana ndio wanaochochea ukatili huu. Pia serikali imeagiza kamati za ulinzi za mikoa kuwalinda albino na pia hivi karibuni imeendesha upigaji wa kura za maoni kwa siri nchi nzima ili kuwabaini wahusika.
Zaidi ya hayo, vyama vya kiraia, vyombo vya habari na hata taasisi za nje pia zimechangia sana katika kampeni hii ya kutokomeza mauaji haya ya kinyama.
Katika mjadala huu, tunakusudia kukusanya maoni ya watu kuhusu nini hasa kifanyike ili kumaliza mauaji haya. Hususan, tungependa kupata maoni yenu juu ya masuala yafuatayo;
Nini sababu (za kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata kitamaduni) zinazopelekea kuwepo kwa mauaji haya?
Unasemaje juu ya jitihada hizi zinazofanyika kuzuia unyama huu (nini zaidi kifanyike?)
Nini majukumu ya Watanzania katika kumaliza tatizo hili?
Je, majukumu ya mashirika ya kimataifa katika kumaliza tatizo hili ni yapi?
Dear wachangiaji katika mjadala huu wa Mauaji ya Walemavu wa Ngozi, ninapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana kwa michango yenu ambayo kwakweli itatusaidia katika kushauri na hatimaye kupata njia sahihi ya kutatua tatizo hili. Nashukuru sana kwa ushirikiano wenu tangu mwanzo wa mjadala mpaka sasa ambapo inatubidi kuufunga ili kupisha mada nyingine.
Aksanteni sana na napenda kuwakaribisha katika mada nyingine zinazoendelea na hata mpya itakayowekwa katika nafasi hii.
Dorah Semkwiji : Thursday, July 16, 2009
Judie Nakubaliana nawe kabisa kwa mchango wako. Polisi jamii inasaidia ana na kwa kweli imesaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti ujambazi hapa nchini. Swali langu ni nini kifanyike ili hii isaidie pia suala la albino? kwa sababu kwa kuangalia juu juu utaona kabisa kuwa polisi jamii haiko that active katika suala hili.... je nini kinazuia? je kuna uwoga wowote kwa upande wa jamii unaowafanya wasishiriki kikamilifu kama wanavyofanya kwenye makosa megine kama ujambazi?
Dorah Semkwiji : Thursday, July 16, 2009
Kaka David Aksante kwa mchango wako. Ni kweli upigaji kura kuwatambua wauaji wa ndugu zetu ni kuchochea chuki. Hivi kuna mechanism yoyote iliyowekwa kwa ajili ya kuzichunguza kura hizo? Pili kama jamii husika bado inaamini kuwa albino ni mkosi je unafikiri watu watajitokeza kweli kupiga kura hizo?
Pili serikali inatakiwa ichukue jukumu laini najiouliza serikali ni nani? Nafikiri ulinzi wa ndugu zetu hawa ni jukumu letu sisi kama familia, kijiji, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla. Katu tusikae bila kuwalinda kwa kusubiri wapelelezi waje watusaidie.
Laiti kama watu wangekuwa na ule moyo wa ubinadamu mimi naamini kabisa kama mtu angekuwa na mtoto au dada/kaka mwenye ulemavu wa ngozi na kumchukulia kama binadamu kama yeye sidhani kama haya yangekuwepo.
nadhani pia kuna umuhimu wa madaktari watoe elimy ya science ya jinsi albino anavyoweza kutokea ili watu waondoe ilw dhana ya mikosi ambayo imejengeka kwa muda mrefu miongoni mwao
Dorah Semkwiji : Thursday, July 16, 2009
rm besha
Nashukuru kwa mchango wako. Kwanza kabisa napenda kukutoa shaka kuwa hapa unaruhusiwa kutumia lugha yoyote kati ya hizi mbili hufungwi na upande wowote.
Pili nakushukuru sana kwa observation uliyoitoa kwenye mchango wa Ms. Alenga. Ni kweli factors alizozitoa Ms. Alenga (culture, taboos e.t.c) zinasaidia sana katika kulielewa tatizo hili kiundani hasa kwenye mtizamo wa jamii juu ya hawa wenzetu lakini nafikiri hizi zinafaa sana katika kufanikisha (facilitate) mauaji haya. Kwamba kwa kuwa ni rahisi kumrubuni mtu akufanya kile ambacho yeye anaamini kabisa kuwa hakina madhara kwa jamii yake (mtu anayetoka katika jamii ambayo inaamini kuwa albino ni mkosi hawezi kuona ugumu katika kumwondoa albino huyo kama atashawishiwa) so nafikiri ndio maana mauaji haya yanatokea kwa wingi kule ambako jamii yake inaamini kuwa uwepo wake ni mkosi mf. Shinyanga, Tabora na Kigoma (kama sikosei)
Tatu unasisitiza kuwa adhabu zitolewe kwa wale wanaohusika. Ni kweli kabisa nami ninaunga mkono kabisa ila najiuliza ni adhabu gani ambay itatoa fundisho> Kwa sababu adhabu iliyotengenezwa kwa wabakaji ya miaka 30 jela inatekelezwa ila bado watu wanaendelea kubaka. Nafikiri hapa itabidi vyombo husika watusaidie
Na mwisho tunaonaje kama uadilifu na usafi ukaanzia kwenye vyombo vinavyohusika na usalama wa raia kwa sababu kama polisi ambaye anatakiwa alinde maisha yangu anadiriki kushiriki katika maovu sipati picha raia watakuwaje? (Mf. Kesi ya kina Zombe!)
Dorah Semkwiji : Thursday, July 16, 2009
Nashukuru sana kwa kuendelea kutoa michango yenu hapa na ninawaomba radhi kwa kutokuwepo kwa muda.
Ms. Alenga thank you very much for your contribution in this matter. Kusema ukweli mchango wako umetusaidia tulio wengi katika kujaribu kutafuta utatuzi wa tatizo hili. Nakubaliana nawe kabisa kuwa mila mbovu ambazo tunaweza kuzioanisha na chanzo cha tatizo hili. However swali la kujiuliza ni hivi kwa nini bado kuna watu wanaendelea kuzikumbatia mila hizi hasa ukizigatia tuko katika karne ya ishirini na moja? Kama ni vitu vinavyojitokeza baada ya kutoweka je nini kinachochea ?
Pili ni kweli kuwa watu tunajenga tabia ambazo tumelelewa nazo (socialization process). Tatizo linabadili mwelekeo pale tunapogundua kuwa tabia flani haiko kwa kabila au society flani tu. Mfano kama mie wamanyema tunaamini kuwa albino ni mkosi iweje wachaga nao waamini the same kama haikuwa kwenye mila zao? (ni mfano tu nimetoa ndugu zangu). Nimesema hivyo kwa kukumbuka ile kesi inayoendelea kule Shinyanga ambapo mshtakiwa alisema kuwa mteja alikuwa ni mwenye asili ya kiasia sasa hii ina maana kuwa mila hizi ziko accross culture?
Yes Irene people need to be educated nakubali but what should be the content? Mode ipi itumike katika kuelimisha huku na je nani hasa ahusike na utoaji wa elimu hiyo- je ni serikali, mashirika ya dini, vyombo vya haki za binadamu au wote?
Albogast Musabila : Wednesday, July 15, 2009
Je ni kweli kwamba Albino wamekuwa wakipotea katika jamii yetu kwa muda mrefu?
Je ni kweli kwamba kupotea kwa albino enzi hizo ilikuwani ahueni ya familia katika jamii kwani albino walikuwa hawakubaliki sana katika jamii zetu kama binadamu wa kawaida?
Je ni kweli kwamba jamii ya wamasai hawana walemavu kwani alipokuwa akizaliwa mtu asiyejiweza wanamwacha ndani ya nyumba na kuhama hilo eneo? Maana ilikuwa ni mzigo kuhama na watu wa aina hiyo....
Kama majibu ya maswali haya ni NDIYO..then hili suala la mauaji ya albino linahitaji mtizamo mpya zaidi ya sababu za kiuchumi na nguvu za dola ambazo ndo zimepewa kipaumbele!!
Hilsen
Musa
Aurelia Kamuzora : Wednesday, July 15, 2009
Nimekuwa nikifatilia majadiliqno yanayoendelea hapa kuhusu unyama huu unaofanywa na wauaji hao. Je chimbuko nini?
Kwa uelewa wangu wa sheria za uchumi na maendeleo. Sheria hutungwa na watu kufuatana na jamii ilivyo. Hata ufuatiliaji wake unafuatana na jamii ilivyo. Kuna mwandishi mmoja anaitwa Jean-Jacques Rousseau ansema-""War is consitituted by a relationship between things and not between persons, and as the state of war cannot arise out of simple personal relationship, but out of real relatios private war or war of man with man can exist neither in the state of nature where there is no constant property, nor in the social state where everythig is under the state of law" .
Hivyo basi, matatizo ya kuua Abino ni vita ya kutafuta mali -"relationship between things". Watu wa Tanzania wamekuwa na umoja na amani. Wameishi na Albino miaka na miaka. Tujiulize kwa nini ili limezuka wakati huu wa Economic crisis iliyoanza makali yake tangu 2007. Je Watanzania hawa siyo wenzetu wenye elimu duni juu ya makali haya? Je siyo wenzetu ambao wanaenda kutafuta mali kwa njia ya Waganga wa kienyeji? Je polisi pekee na upelelezi wa dola unatosha kumaliza tatizo hili?
Mimi nafikiri kunahitajika kufanya kongamano kuangalia ni jinsi gani tunaweza kuelimisha jamii kuondokana na kutegemea sana ramri, kamali , utabiri usio na tafiti za kisayansi na mengineyo. Tunachokiona leo ni matatizo ya muda mrefu ya kuwaita mama wazee wenye macho mekundu wachawi, kuwakata mikono watoto wadogo, kutambika watoto ili kutafuta mali .n.k.
Kwa vile waganga wa kienyeji bado wanaendelea kufanya-innovations zao kwa kuwadanganya watu wanaotafuta mali kwa nguvu.,tatizo hili bado ni kubwa. Albino wakiisha waganaga wa kienyeji watatafuta njia nyingine ya kupata mali. Zamu hii watatutafuta sisi tunaochangia kwenye TAKNET!!!.
Mimi naona serikali iwatafute waganaga wa kienyeji wapewe hospitali zinazoeleweka. Wajirejiste na watoe vibali na prescriptions kwa wagonjwa wao. Waeleweke wanachofanya. Ikibidi wa-specialize. Wafanye kazi na madaktari wetu wanaotumia tafiti za kisayansi kama wanavyo fanya nchini China. Wananchi waeleweshwe kuwa kinachotibu kwa waganga wa kienyeji ni dawa siyo ramri.
Tukiweza hapo tunaweza kushinda vita hivi. Vinginevyo, baada ya Albino , vitatafutwa vichwa vya wasomi-maprofessor , viongozi wa zamani, ngozi ya wabunge, n.k. Kinachogomba hapa ni umaskini wa ulewewa. Polisi hataweza kumaliza hili tatizo kwani yeye atalala kila mahali? Elimu duni ndiyo tatizo kubwa. Sheria bila kuwa ya ki-tija (efficiency of law compliance) hatuwezi kushinda. Watu watatafuta njia nyingine ili wapate vichwa vya mtu au Albino.
Tutafute suluhisho endelelevu. Mfano mzuri ni tatizo la vibaka. Mbona wananchi wenyewe wameweza kuchukua sheria mkononi na kupambana nao, hata kama siyo vizuri. Je sheria mkononi zitamalizwa na polisi. Kama sheria hazitungwi kwa kuangalia uwezekano wa kuzi-enforce, tunajidanganya. Tuelimishe jamii na kuweka mikakati ya kuifanya jamii ielewe kuwa mali hutafutwa kwa kutumia akili na juhudi siyo kuwachinja Albino wala kukata vichwa vya nyani wala kutoa kafara..
Hao Waganga wa jadi waandikwe na tujue wako wapi na wanafanya nini. Jamii eleimishwe kuwa mali hutafutwa kwa kufanya kazi. Tuna Redio, serikali inaweza kupeleka vipeperushi kwenye mashina n,k. Hili ni tatizo kubwa la uelewa , haliwezi kumalizwa na polisi peke yake. Wananchi gani washirikiana na polisi, iwapo ndio wanashinda kwa waganga wa kienyeji wakitafuta mali?
Samahani kwa kuwaandikia barua ndefu. Hicho ndicho kifanyike.
Aurelia Kamuzora
PhD-Fellow (Law and Economics)
Groningen University
Netherlands
Julie Adkins : Wednesday, July 15, 2009
Nakubaliana na Ndg. Chitumbi. Uaji ni kosa la jinai hata kama ni aliyeuawa ni Albino au mtu yoyote yule. Kazi ya kuwatafuta, kuwasaka na kuwakamata wauaji ni kazi ya polisi, upelelezi na vyombo vingine vya serikali.
Inaonekana kuwa mfumo wa ‘polisi jamii’ (community policing) umeanza kuleta mahusiano mazuri zaidi kati ya jamii na polisi wenyewe. Nadhani polisi wangepata ushirikiano zaidi na jamii kuhusu suala la mauaji wa Albino kama wangeendeleza mfumo huo.
Asante
Julie
David Chitumbi : Monday, July 13, 2009
Ndugu zandu nawasalimu!
Kupiga kura kuwabaini wauaji wa Albino ni sawa na kuchungulia chumba chenye pazia la chuma. Kwa kifupi kile ni kiini macho na ni chanzo cha chuki katika jamii.
Mi nadhani kwa kufanya hivyo serikali dhahiri imeshindwa kazi yake. Nchi ina rasisilimali watu kibao ikiwemo idara ya upelelezi na hata usalama wa Taifa, iweje idara zote hizi zisifanye kazi yake ipasavyo?
rm besha : Monday, July 6, 2009
dear members,
once again it is nice to be here...the last contribution was in english so my mind is now in a dilema,calculating whether i should contribute in english or swahili,but since my question and/or contribution is/are meant for miss alenga,it should be fair enough to use english....
i think what miss alenga has contributed,has been of utmost impact in a sense that maybe the killings are decided upon under the influence of culture-the passed down values, taboos, practices, etc as she puts it.but then again,do these millionaires who pay for and orchestrate the killings belong in the sphere encircling those on which the values have been passed?is it our leaders?ourselves;tanzanians?is it the albinos themselves?are we not past this line of thinking and living?or does it still have so strong an effect on some of the filthy rich or amongst ourselves?
many questions arise here,and yes miss alenga,people need to educated here,from the grass roots that is,but as for those who are so deep into these beleifs that it's got them killing fellow innocent tanzanians, and those who are supposed to be watchdogs, action needs to be taken and justice served so that we all keep in mind that such despicable cruelty is not tolerated and is far from culture,values,beleifs or anything else of that sort! this will be a great first step towards preventing further killings…
akhsanteni.
IRENE ALENGA : Thursday, July 2, 2009
All deviant behavior can be traced from our socialization processes, what is acceptable or not in a society is made so through years of passing on of values, cultures, taboos and practices on social relations. True, African culture has been in time considered as having grotesque practices and this is (according to my opinion) due to what we deem as abnormal and ways of creating normality. Twins were considered a taboo in the old days in many communities, FGM was for some communities considered as a rite of passage for which a female not having gone through it would be exorcised from the community, HIV/ AIDS was considered as a curse and one would be exiled from society, all these are forms of victimization due to lack of understanding of strange occurrences in society… what then should we do to stop this? Nip it at the bud…Education is the key to success! Interject through the leaders and elders in society or the practitioners of these killings and even evoke harsh punishment to anyone who is found guilty as an example to evoke fear and as a result deter future practices. Educate at all levels to ensure that everyone is aware and make it a civic responsibility of individuals to hold precious what it is that they value so dearly .. LIFE!
So I throw the ball right back to your court (especially the English speaking people on this forum) what is your view on this issue? Has enough been done? Are there any recommendations on mitigating options to solve the problem?
IRENE ALENGA : Thursday, July 2, 2009
I would like to thank you all for joining this forum and giving a lot of helpful information and insights on this very sensitive topic. i would like to break it down for the members within Tanzania and outside our borders on the interesting insights that you have contributed in the last two and half months that this topic has been up for discussion.
I believe this is a stain to the general friendly, social and welcoming demure that our people are known for all over the world. Indeed we all received the news in the international arena with shock; I for one was very concerned of the practice.
Following the briefing note introducing this topic many of you have looked at the major causes or if I may say influencing causes of these killings as economic, socio-cultural and even political given that most have mentioned belief in the use of these body parts as a catalyst to wealth, popularity and success of the persons practicing in the faith of these killings. Some have even suggested cult practices by some religions and traditional belief systems.
Dorah Semkwiji : Friday, June 26, 2009
Ndugu Besha, ntunashukuru sana kwa mchango wako mzito. Kwa kweli umeelezea vema kabisa na ni wajibu wetu sisi kama watanzania tuzingatie haya unayoyaandika. Suala la umasikini umeelezea vema na kama nimekupata vizuri ni kwamba umasikini ndio unaopelekea watu kukubali kufanya mauaji haya.
Kwetu imekuwa rahisi kwa mtu kurubuniwa ili alete mkono au mguu wa binadamu mwenzake!! tunatia aibu ila swali langu hapa ni nani anayewarubuni hao wauaji? Kutokana na kesi ya mauaji shinyanga inavyoendelea, ni wazi kuwa wafanyabiashara wakuu wanawarubuni watu masikini kufanya hayo mauaji je wafanyabiashara hawa wanatumwa na nani viungo hivyo?. Ni waganga au kuna sehemu nao wanakwenda kufanya biashara?
Pili umezungumzia suala la umasikini wa wenzetu albino. Kusema ukweli ukiangalia albino wengi wako vijijini na wanaishi maisha ya shida kama ulivyotuelezea ila tulishajiuliza ni kwa nini? Hii haitokani na unyanyapaa ambao tumekuwa nao dhidi yao kwa muda mrefu? Fikiria mtoto anayezaliwa akiwa na ulemavu huo wa ngozi, ni mazingira gani ametengewa ya kumwezesha kusoma na kufaulu vema? kwa sababu tukubaliane kuwa elimu bni ufunguo wa maisha na ni imani yangu kuwa kama hawa wangesoma na kuipata ile elimu wanayoipata wengine basi wengi wangekuwa ma-CEO kwenye office mbalimbali, mawaziri na viongozi wengine nchini.
Kwa mantiki hii basi nafikiri bado kuna haja ya kuwapatia special attention hawa wenzetu ili kwanza kuwasaidia hawa waliopo kwa kuwalinda na kuhakikisha tunawatengea mazingira mazuri ya elimu ili kuwakwamua na umasikini wao. Pili kuna haja ya kuifanya mipango hii kuwa endelevu kwa sababu naamini kabisa kuwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaendelea na wataendelea kuzaliwa tuwalinde kwa kuwajengea mazingira mazuri ya elimu na maisha kwa ujumla. Ninaamini kabisa Albino aliyejikamilisha kwa elimu, kazi, mahitaji muhimu na ufahamu wa kutosha juu ya ulinzi haitakuwa rahisi kwake kuuwawa na wahalifu hawa ukilinganisha na yule wa kijijini.
rm besha : Friday, June 26, 2009
habarini za leo ndugu zangu,
kama ilivyo ada,nimefurahishwa sana na mawazo yanayotolewa kwani yanagusa kila kona ya tatizo.kwa kusoma juu juu tu,nimeweza kuona maneno yaliyotawala sana ni hali duni,siasa, ujinga na uzembe au kutojali. hizi zaweza kuwa ni sababu kubwa sana zinazosababisha mauaji haya..
kwa kuanza tu na hali duni,watanzania wengi waishio vijijini wanaishi maisha ambayo ni ya taabu na shida mno kama ilivyosemwa na wachangiaji wengi hapo awali,wengi ni watu ambao noti ya elfu kumi kwao ni kama milioni moja kwetu sisi wenye kipato cha kawaida au cha chini ila cha halali...ninachotaka kusema ni kwamba mtu mwenye maisha kama haya ni rahisi sana kupokea milioni ili auwe jirani,mtoto mke, mume na kadhalika,swala lingine hapa ni kwamba hawa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi wanaishi maisha ya tabu sana,macho hayaoni vyema,ngozi inaharibika vibaya juani na wengi ni masikini,kwa namna moja ama nyingine inawezekana kuna hisia kwamba hawa watu hata wakiuwawa/tukiwaua ili watajirishe watu,tunasaidia kuwapumzisha maana hapa duniani maisha wanayoishi ni ya shida..hii inaashiria kwamba wametupwa na hawajaliwi….
-swala ni kwamba watanzania tumepoteza utu, huruma na hatujali wenzetu, na wengi wetu ni masikini ambao twaweza kufanya chochote ili tupate fedha za kujikimu au utajiri wa haraka ila hapahapa ninajipinga mwenyewe maana ninaamini kwamba,wapo masikini wa hali ya chini kabisa ambao hawawezi kuua hata mtu wasiyemfahamu ili watajirike..swala la kuua au kukata watu mikono ni roho mbaya na chafu za watu wachache...ila umasikini na wenyewe unachangia kwa sababu tofauti kati ya masikini na matajiri hapa tanzania(disparity) ni kubwa mno,kama wengi wetu vijijini na mijini tungeishi maisha ambayo hayatofautiani kwa kiasi kisichoweza kuaminika,haya mauaji yasingekuwepo... angalia namna ambavyo baadhi ya viongozi wetu wanaishi kifahari,na kwa upumbavu wetu tunawatukuza na kuwasifu,heshima wanapewa wenye pesa bila kujali zimetoka wapi…nani asiyependa kuheshimika?hakuna asiyetamani maisha haya…hapa ndipo watu wanapoamua kutumia nguvu za kishirikina ili watajirike..
kwenye swala zima la siasa,kama ilivyokwishasemwa,kumshambulia mh. pinda kumedhihirisha wazi ni namna gani viongozi wetu wanajali kutengeneza majina kuliko kutatua matatizo ya wananchi wao...hapa ninawaambia wote look around you! ni watu wangapi ofisini kwako unaambiwa wana”jikoki” ili wasipoteze nafasi zao,unaambiwa usikorofishane na Fulani, atakukaanga, ni viongozi wangapi tunasikia wanaingia madarakani kwa ushirikina? wa serikali mpaka wa dini...ninaambiwa kuna hirizi zinasindikwa kwenye altare makanisani ili bwana kiongozi wa dini asiondoke kanisani hapo, asishushwe cheo au asilogwe...vicky mtetema wa bbc alisema wazi kwamba kati ya watu waliyokwenda kuona waganga wanaofanya vitendo hivi ni maafisa na mapolisi wa vyombo mbalimbali vya dola,hawa ndio watu tunaowategemea kulinda usalama na kufanya uchunguzi wa matukio kama ya mauaji ya albino.je,kama wengi wao ndio mambo wanayoyakumbatia na kuamini ndio yanayowalinda,watayachunguza au kujali?kama hili lipo pia ndani ya 'usalama wa taifa', kuna chochote kitafanywa?
nilishangaa na kuumia sana nilipoona kwenye taarifa ya habari wale wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa (international community) ambao walikuja nchini kuhakikisha haki inatendeka..na walisema wazi,tumechoka kuambiwa ‘tunafanya uchunguzi, hakuna linalotendeka ’ na hatuondoki mpaka tuone watu wanachukuliwa hatua..watanzania tuko wapi?kweli wageni wana uchungu kuliko sisi?tunapoteza muda mwingi kwenye vijiwe tukilalamika serikali haifanyi kitu, tunaongea kwenye tovuti kama hii ya taknet lakini hakuna la zaidi tunalofanya...hapa nasema wazi kwamba sisi tumewaangusha wenzetu walemavu kwa kukaa na kuongea kimbeya huku mauaji yakiendelea..siku zote nguvu ziko mikononi mwa wananchi wenyewe......
mahakamani nisingependa kuona wauaji tu wakipandishwa kizimbani,hatujui walikuwa na hali gani wakati wakiua,kama swala zima linahusiana na nguvu za giza, si ajabu walikuwa 'possessed'-yaani pasipo ufahamu wao walifanya mauaji hayo;ni maneno yangu tu,ila ningependa kuona wale waliyowatuma waue,wanaotoa haya mamilioni, na watumiaji wa hivi viungo ndio wafikishwe mahakamani na wapewe adhabu wanayostahili...tatizo la mauaji ni pana mno,ni mengi sana inabidi yaangaliwe…kuanzia utendaji, sheria, misimamo na mitizamo ya watanzania, utu na kadhalika!
akhsanteni.
Dorah Semkwiji : Friday, June 26, 2009
Kaka Massawe kwanza tunapenda kukukaribisha katika jukwaa hili la elimu. Aksante kwa kushiriki nasi katika mjadala huu. Napenda kuungana nawe katika ushauri ulioutoa. Ni wazi kutokana na jinsi vyombo vyetu vya usalama nchini vinavyofanya kazi ni wazi kabisa tukitegemea viwe ndo walinzi kwetu tutaumia.
Ongezeko la maovu nchini ni wazi kuwa kuna walakini katika utendeji kazi wao. Nimekuwa nikifuatilia matukio ya mauaji ya kinyama ya waendesha pikipiki nimesikitishwa sana. Ina maana wauaji hawakamatwi wala watu wanaoshukiwa na lawama badala yake zinapelekwa kwa waendesha usafiri huo!!
Ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi, sisi, mimi na wewe ndio walinzi wakuu. Inatubidi turudi katika ile jamii ya zamani ambayo mtoto wa mwanakijiji au mwanajamii ni mtoto wa kijiji au jamii nzima kwa maana ya kwamba wanakijiji au wanajamii wote walikuwa wanachukuliwa kama ni wazazi wa huyo mtot huivyo waliweza kumkanya na kumwadhibu pale anapokosea. Albino wanatakiwa kulelewa katika jamii ya aina hii ambapo wanajamii wote watawachukulia albino kama watoto, kaka, dada, wazazi wao na si kama jirani au mtoto wa nyumba ya pili!
James Mazigo : Friday, June 26, 2009
Kuna mtandao unaitwa FREEMASON.Kwa taarifa ambazo siwezi kuthibitisha, mtandao huu ambao kwa namna flani ni wa kiimani,wamekuwa wakifanya matambiko na kuendesha mikutano/ibada ambazo katika kutoa kafara hu-usisha kutoa uai wa wanadamu.Narudia kusema,sina taarifa kamili/rasmi lakini nashawishika kukubali.
Hoja yangu sasa ni hii inayofuata;kwamba katika ibada hizi za kishetani za mtandao huu,wanachama ama waumini,pamoja na wengine wengi,mara nyingi ni wafanyabiashara wakubwa,viongozi wa ngazi za juu serikalini,eti hata baadhi ya viongozi wa juu katika baadhi ya makanisa,masinagogi,'temples' nk!Ikiwa hivi ndivyo,mzizi wa ushetani haung'olewi kilelemama.
Ni kweli juu ya usemi wa lugha ya Kiswahili,KESI YA NYANI KAPELEKEWA TUMBILI!Pengine ni vema kujua kwamba adui yako ni unaemwona kuwa rafiki yako.Ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi watambue kuwa hakuna njia moja na pengine si rahisi kudhibiti uasi juu ya ngozi zao.Tutasaidiana ndio, lakini hatima ya usalama wao iko kwa Mungu na wao wenyewe.Mzizi si rahisi kuupata na kuung'oa.
Watanzania tujue kuwa unyama/ushetani huu unaanza mbali sana.Ni vema tujue ukubwa wa tatizo na tusiadae nafsi kana kwamba hili ni jambo la kudhibitiwa kilelemama.
DEOGRATIUS B. MASSAWE : Friday, June 26, 2009
Nimefurahishwa sana na jinsi walivyochangia wanachama wengine kwenye hili suala la mauaki ya kinyama ya haya ndugu zetu maalbino na wengi wanahusisha matukio haya na ushirikina.Jutokana namili nashauri yafuatayo;
Tujaribu kuwapa ulinzi wa kutosha na hasa jamii inayowazunguka kwa maana vyombo vyetu vya usalama haviko committed ana pia havina uwezo wa kutosha kuhakikisha ulinzi.
Pia, mashirika mbalimali kama NGO's yajaribu kuwapa msaada hasa watoto na wanawake ambao wengi wako vijijini bila ulinzi wala misaada yeyote
Mwisho tunaitaji kuufanya uchunguzi wa kutosha kwa wanakamatwa ili yujue viungo iuvyo vinhatijika wapi na kwa matumizi gani.Mana bila kujua chanzo ni kazi bure tu
Dorah Semkwiji : Thursday, June 25, 2009
Kaka Mazigo Hapa umetufumbua macho wengi. Pamoja na kuwa umesema kuwa huna uhakika na hayo ila kama ni kweli basi nidhahiri kuwa tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu kama tutaamua kuwaadhibu wauaji wa albino bila kujua chanzo chake ni nini. Iwapo hawa akina Freemason kweli wapo basi ni wazi matukio haya ya uuaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi na mengine ya kutisha zaidi yataendelea kuwepo na baadae tunaweza tukaja kushuhudia mabaya zaidi. Nafikiri kuna haja ya serikali kupitia na kuzitafiti hizi dini nyingine zinazoibukia kila kukicha.
Wasi wasi wangu ni kuwa isijefika wakati tukajikuta tunakuwa na taifa linaloongozwa na dini za kishetani ambazo masharti yake ni kutenda uovu kwenye jamii.
Dorah Semkwiji : Thursday, June 25, 2009
Aksante sana ndugu Kilewa kwa mchango wako mahususi juu ya tatizo hili. Mimi kaka mimi nakubaliana na wewe kuwa serikali haijaonyesha utayari wake katika kulivyalia njuga suala hili. Ni jambo la kushangaza kwamba inapofikia issue hii wengi wetu tunanywea kama vile kuna kitu tunahofia. Najaribu kufikiria uwezekano wa police kuweza kuwasaka wahalifu mbalimbali na kuwatia nguvuni lakini kwa suala hili la albino imeshindwa. Je serikali inataka tuamini kuwa hili lio nje ya uwezo wetu? au kuna umuhimu wa kuwaomba Interpol watusaidie katika hili? Mbona kwenye kipindi kile cha Forensic tunaonyeshwa jinsi ambavyo the impossibles are being brought to the possibilities?
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini kesi iliyofunguliwa kule Shinyanga na Kahama dhidi ya wale waliokamatwa kwa kosa la kuua albino kwa kweli ni vitu vya kuhudhunisha. Ila bado najiuliza je hao tu ndio waliopatikana na makosa haya? au bado wengine hawajafunguliwa mashitaka? Kwa sababu kwa kumbukumbu zangu mauaji haya yametokea pia Kigoma, tabora na hata Bukoba ila huko sijasikia bado kama kuna mtu amefunguliwa mashitaka au uchunguzi bado unaendelea au wauaji hawajapatikana?
Serikali tunaomba mtutoe gizani
NOTKER P KILEWA : Wednesday, June 24, 2009
Awali ya yote,napenda kuwashukuru wachangiaji wote waliotangulia.hii inaonesha jinsi gani watu wapo makini na masuala yanayowazunguka.
mchango wangu juu ya tatizo la walemavu wa ngozi ni kwamba.kwanza serikali pamoja na wananchi wote tunatakiwa tujue mtandao mzima unaojihususha na biashara hiyo haramu pengine kuliko hata zile zilizo zoeleka kuitwa haramu.
kinachoonekana hapa ni kwamba serikali inashughulika zaidi na wale wanaokamatwa kwa kuua wenzetu hao,bila kuchunguza kwa umakini chanzo au wale wanaowatuma.
ikumbukwe kuwa mtandao huu unahusisha matajiri au wale wanao hitaji viungo,waganga wa kienyeji,majirani wa hao wenzetu ambao ndo wanachora mpango mzima na wauaji wenyewe.
tunatakiwa tukumbuke ule msemo wa kikulacho ki nguoni mwako.wakati mwingine hata watu wa karibu na albino wanawauza ndugu zao kwa tamaa ya pesa.
kama ilivyo kwa uhalifu mwingine.pesa kwa mfano ambapo majambazi wanapata taarifa kamili ya kiasi cha pesa ,muda wa kusafirisha,sehemu zitokazo na ziendako.habari zote hizi hutoka ndani ya wahusika wa financial institution inayohusika kwenda kwa majambazi.
hali kadhalika mauaji ya albino yanawezeshwa na taarifa wezeshaji toka kwa watu wa karibu.hivyo hayo yote yatazamwe.
Dorah Semkwiji : Wednesday, June 17, 2009
Kaka Mbundi aksante sana kwa mchango wako. Kwa kweli uliloandika hapa ni kweli kabisa. Hatuwezi kuzuia mauaji ya albino kwa kutumia nguvu bila kujua wale tunaowazuia wana mtazamo gani juu ya albino.
Ni wazi kuwa suala hili linatakiwa kuangaliwa kwa mapana zaidi na si kukurupuka tu na kura za maoni. Umuhimu wa kujua mtazamo wa watu juu ya wenzetu hawa ni mkubwa ni sawa na kujaribu kupunguza UKIMWI nchini bila kuzungumzia suala la unyanyapaa (stigmatization).
Kama jamii inawanyanyapaa albino basi haitaweza kuwa na uchungu kuona wanauliwa ovyo. Tunahitaji kujua mtazamo wao na kisha tuanzie hapo kama ni mtazamo potovu unaowanyanyapaa albino basi tuanze kwa kuubadili uwe mtazamo chanya ili kuweza kupata nguvu ya pamoja katika kupigana na mauaji haya!!
kwa hisia za juu juu tu, tunafikiri nini mtazamo wa watanzania walio wengi juu ya uwepo wa wenzetu hawa?
stephen Mbundi : Wednesday, June 17, 2009
Ni ukweli usiopingika kuwa mauaji ya albino ni aibu kwa nchi yetu na sio muafaka kwa wanasiasa kudandia suala hili kujitafutia umaarufu. Sipendi kukubali sana hoja ya kupiga kura ili kuwapata wauajiwa albino japokuwa hatua hii inaweza kupunguza tatizo au kuahirisha tatizo lakini sio kulimaliza.
Nakumbuka wakati wa utawala wa awamu ya kwanza katika mikoa ya wafugaji waliwahi kupiga kura kuwatambua wezi wa mifugo, na wale waliopata kura nyingi walihamishiwa mikoa ya kusini lakini tatizo leo lipo pale pale aidha ushahidi wa kimahakama utapatikanaje?
Kwa mtizamo wangu, mauaji ya albino ni suala la kihistoria zaidi na linahitaji mtizamo mpana kuliko kuangalia sababu za kiuchumi. Mauaji haya yamekuwapo na yamekuwa yakifanyika kwa albino tangu wakiwa watoto wachanga kwa kuamini kuwa hawatakiwi katika jamii. Tumekuwa tukisikia hata wazee wanadai kuwa albino hafi bali hazikwi na ndio maana ukiuliza watu wengi iwapo wanatambua kaburi la albino ninaamini itakuwa mwanzo wa hadithi nyingi zitakazokuchanganya. Hivyo ili kuzuia juendelea kwa tatizo hili ni bora kwanza wataalamu wa masuala ya jamii wakafanya utafiti kujua: 1.jamii zetu zina imani gani juu ya kuwepo kwa albino miongoni mwao; 2.nini imani yao juu uwepo wao; 3.Ijue jamii ina uamuzi gani kuhusu albino katika jamii zao
Baada ya hapo ndipo mkakati kamambe wa kuondoa imani kwa kushirikisha wazee wa jadi na wasomi ifanyike. Nguvu ya dola pekee haitosaidia kwani hili ni suala la imani. Tusiwaangalie wale tu waliobahatika kuwa watu wazima wakauawa kuna wengi ambao hawafikishi hata wiki kabla ya kuuawa. Nakumbuka kuna kiongozi mmoja aliwahi kusema alipewa pole na waziri mmoja wa nchi fulani kwa jinsi tatizo la albino linavyochafua jina la nchi yetu, akamuuliza nyie kwenu halipo tatizo hili? alijibiwa kuwa halipo kwa kuwa tunawaua wakiwa wachanga hivyo hakuna anayeona, tatizo Tanzania mnaawacha wanakua ndipo mnawaua. Hii ni ushahidi kuwa hili ni tatizo la kihistoria na sio one time event
Dorah Semkwiji : Friday, May 29, 2009
Kaka Makongo ni kweli kabisa usemayo na ni wazi serikali inawajibu wa kutuambia matokeo ya hizo kura za maoni na hata kama zoezi zima halikufanikiwa walipaswa pia watueleze wananchi. Lakini tujiulize pia serikali na nani? Mimi nafikiri sisi wananchi ndio serikali kwa sababu tunapaswa kuwa aggressive katika kudai haki zetu. Ninaamini kabisa kuwa kama tutasimamia kidete kutaka matokeo hayo yatolewe basi tutaweza kuyapata au?
Hivi wakati unapitishwa uamuzi huo wa kura za maoni wananchi walihusishwa kikamilifu? Kwa sababu kama walihusishwa ni wazi kuwa hata wao waliafiki na kuona kuwa hii ni njia nzuri ya kukabiliana na tatizo hivyo ningetegemea ushirikiano wao hapa uwe mkubwa (hasa kwenye hizo kanda zilizokuwa zimeteuliwa). Na kama wangeshiriki ni wazi tungepata matokeo yake)
Lakini kama agizo hili lilitoka juu na kuwa imposed kwa wananchi kama sheria bila kuwashirikisha wao basi tusitegemee lolote kwa kuwa hata wapiga kura wenyewe hawatajisumbua kuhangaikia kitu ambacho hakijatoka mioyoni mwao kwa utashi wao.
Asasi zinazotetea haki za binadamu nilitegemea zingelifanya tatizo hili kama agenda kuu na kulishikia bango hadi tujue mwisho wake lakini kwa masikitiko yangu imekuwa ndivyo sivyo. Baada ya kuanzishwa kile kituo cha Under the Same Sun nafikiri (tena tumesubiri kikajakuanzishwa na mkaazi wa nje ya nchi) hakuna kilichoendelea zaidi ya vile vya kuwawezesha albino kiuchumi kama kutoa mikopo ambapo swali la kujiuliza ni huyo albino atatokaje kuupata huo mkopo, atauinvest vipi mkopo huo wakati wauaji wanatishia uhai wake?
TGNP, TWLA, LHRC, WLAC mko wapi?
inanisikitisha jinsi suala la malumbano kati ya viongozi wa kisiasa zinavyopewa vipaumbele kuliko suala hili la uhai wa binadamu. Waandishi wa habari wetu ni wafuata upepo, tungeweza kumpata hata mwandishi mmoja atakayefuatilia suala hili na hatua zilizofikiwa ni wazi tungepiga hatua kubwa katika kupambana na ukatili huu but now wote wameshasahau kama kulikuwa na wimbi hili lililodhulumu maisha ya ndugu, jirani, rafiki na wapendwa wetu ambao kwa uumbaji wake MUNGU wamezaliwa na ulemavu wa ngozi.
Suala hili limekuwa ni suala lao (albino) na wala halituhusu sisi (wenye ngozi zisizo na ulemavu).
Inasikitisha.
japjet Makongo : Friday, May 29, 2009
Umetukumbusha saula la kura za maoni. Kama kweli serikali iliona hii kama njia ya dharura....ni lazima watoe matokeo ya kura hizo mapema ili kijenga imani ya wananchi kuwa walikuwa na dhamira. Sasa nani wa kufuatilia...tupige kelele...
Asasi zinazotetea haki za binadamu WLAC, TWLA, LHRC, TGNP,nk zimekaa kimya
Makongo
Dorah Semkwiji : Monday, May 25, 2009
NOVATUS KARIBU SANA KATIKA UWANJA HUU WA ELIMU. Nimefurahishwa sana na namna ulivyolichambua suala zima la Mauaji ya Albino Tanzania. Ni ukweli usio pingika kabisa kuwa wengi tunauelewa tofauti wa tatizo hili na ndio maana tunajikuta na tafsiri nyingi za tatizo hili.
Kwa wewe ulivyochambua jinsi wana taaluma mbalimbali wanavyolitafsiri ni wazi kuwa hata njia za kutatua zitatofautiana mfano kwa maelezo yako wewe Mwanasheria atasema utatuzi wa tatizo hili umelala kwenye kuangalia upya sheria zetu na kuzifanyia ukarabati au kutunga sheria mpya zitakazolenga katika kutatua tatizo hili na vivyo hivyo watu wa mila na tamaduni ambao wanaamini kuwa kupata mtot albino ni mkosi atakupa njia nyingine za kutatua tatizo hili.
Kwa hiyo ni vizuri kwanza kwetu kujua ni tafsiri ipi tunayolenga kuitumia.
Kwa hiyo kama alivyoshauri Novatusi ni vizuri tukafanya tafiti mbalimbali juu ya hili si kwa ajili ya kupata takwimu sahihi tu bali kupata haki ya kulizungumzia kama tatizo. Hii ni kwa taasis zote zinazohusiana na mambo ya jamii, haki za binadamu na elimu pia.
Kwa mujibu wa Afisa Habari Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Othuman Othuman, taarifa rasmi za matokeo ya kura za siri za kuwabaini hao wauaji wa albino,kuwabaini majambazi na wauza dawa za kulevya nchini ambazo zilianza kupigwa tangu mwezi Machi mwaka huu bado hazijafika kwenye Wizara hiyo ambayo ndio wizara inayotakiwa kuyashughulikia.
Hali hii imepelekea baadhi ya wanasiasa kudai kuwa kura zile zilikuwa danganya toto ya serikali katika kuwafanya wanachi waiamini kuwa inashughukia matatizo yao hasa katika kipindi hiki tunachoelekea uchaguzi mkuu.
Swali langu ni kuwa kama kuna ukweli katika madai haya? na kama ni ndiyo je kuna haja ya kulitizama tatizo hili kwa dhana ya kisiasa?
Novatus : Tuesday, May 19, 2009
kwa mara ya kwanza katika mtandao huu napenda kuchangia juu ya mada hii na pia kujtambulisha. kwa jina naitwa Kaijage Novatus na taaluma yangu ni Maendeleo ya Jamii.
swali kuu katika mjadala huu ni nini kifanyike? kwa maana ya kukomesha mauaji ya Albino. yawezekana mchango huu unakuja wakati si wenyewe sana maana kwa sasa matukio yamepungua. lakini masuala ya msingi katika hoja zangu ni mawili. La kwanza nini mtazamo wetu tunapoangalia tatizo na pili tatizo tunalichanganua vipi? ninaposema mtizamo naangalie taaluma mbalimbali zinavyoangalia matatizo/uharifu katika jamii.
Mfano mwanasheria naamini ataonakuwa suala hili lipo kwa sababu aidha sheria hazijafanyakazi vizuri au hakuna sheria za kudhibiti vitendo vya namna hii. Kwa waumini watasema huyu ni shetani ameingia na tunahitaji kutubu na kumrudia mungu.
kwa wale wanaopenda tamaduni zao watatwambia maana ya kila tukio kwenye jamii linamaanisha nini, watatueleza juu ya nini kifanyike wakizaliwa watoto mapacha,watatwambia mira zilikuwa zinafaya nini akizaliwa mtoto albino katika familia na mambo kadha wa kadha. wasosholojia wanaingalia jamii kama mwili wa binadamu. wanaona jamii kuwa ina viungo kama mwili wa binadamu ulivyo.
jamii ina kichwa, kiwiliwili,miguu n.k hivyo kama kuna tatizo kwenye jamii basi kuna moja ya kiungo au viungo vimeshindwa kufanyakazi. viungo ambavyo wanasoshojia wanaviangalia ni pamoja na familia,utamaduni,elimu,dini,siasa na uchumi.viungo hivi pia huitwa taasisi za kijamii.Huo ni mtazamo mmojawapo wa kuangalia suala hili lakini kwa upande wa pili ni uchanganuzi wa tatizo lenyewe.
naamini mauaji si tatizo bali ni matokeo ya tatizo sasa tatizo ni nini?
wataalam wanasema kama hujafanya utafiti basi si vizuri sana kujenga hoja maana yatakuwa ni mawazo yako na hisia zako binafsi zinavyo kutuma. hivyo tunahitaji kufanya utafiti wa kutosha kabla hatujasema nini kifanyike.
Katika kutafiti ni vema tutafute mizizi ni hipi? shina ni lipi? na matawi ni yapi? mizizi,shina au matawi tutaweza kuviona katika zile taasisi za kijamii. mfano familia zetu zikoje? tamaduni zetu zimjengwa na nini na zinatufundisha nini? elimu yetu ikoje na inatujenga vipi? dini zetu zikoje? uchumi nao vipi?siasa ni ya namna gani? hii jamii ambayo
wasosholojia wanaifananisha na mwili wa binadamu viungo vyake viko sawasawa? naliangalia suala hili katika mapana ya kulijadili kwa kuwa nachelea kusema moja kwa moja kuwa tatizo ni hili kwa kuwa sijafanya utafiti wa kutosha na hapo mimi naona ndo pa kuanzia ili kutoa majibu ya kujitosheleza tunapokabiliana na matatizo ya kijamii katika maisha yetu.
watafiti wetu wanapochunguza jambo kama hili wanaliangali kwa mtazamo pana wa kuhusisha sekta zote? au linaangaliwa kipolisi zaidi? yawezekana jibu la kipolisi ni muhimu kwa kusitisha mauaji yasiendelee lakini tunahitaji mikakati zaidi ya kulishughulikia mizizi ya matatizo yetu.
Ni vema tuheshimu zaidi tafiti, tuzitengee rasilimali za kutosha na maamuzi yetu mengi yazingatie tafiti zinatwambia nini.
Dorah Semkwiji : Monday, May 4, 2009
festo thank you kwa mchango wako. ni kweli kabisa kuwa tatizo la mauaji ya albino ni kubwa kwa kuangalia mapana na marefu yako.
Leo tunapoadhimisha siku ya maalbino serikali yetu haijaweza kutuma mustakabali wa wale wote waliokamatwa na either viungo au mauaji ya albino.
Hali hii inavunja sana moyo kiasi kwanmba watu wengi wanaamini kabisa kuwa hakuna kinachofanyika hakuna sheria. Zaidi nimesikia kuwa kumetangazwa mpango wa kuwapatia walemavu wa ngozi (na wengine wote) matibabu ya bure jamani why now? Ina maana hatukuwa tunajua kuwa albino wapo? kwa nini offer hii ije wakati huu?
kwa sasa hivi nadhani hawa wenzet (walemavu wa ngozi) wanachotamani kukisikia ni kuwa mauaji yao yamekomeshwa na wao wako huru kuendelea na maisha yao ambayo yalikuwa yamekatishwa kwa hofu ya kuuwawa.
Na katu si habari za kupewa matibabu bure wala kugaiwa mikopo ya biashara, watafanyia wapi biashara hizo ilhali maisha yao wako hatarini? atatoka vipi akauwekeze huo mkopo wakati kisu, panga, mshale, mkuki na hata bunduki vimetegeshwa mlangoni vikingojea afungue mlango vimmalize?
Tufikirie upya
Dorah Semkwiji : Monday, May 4, 2009
Ndugu Japhet Maingu, napenda kukushukuru sana kwa uchambuzi uliotupatia.
Kusema kweli umeichambua vema na kuonyesha kwa mapana wapi tulikotoka na wapi tunakoelekea katika suala zima la matukio ya ajabu ikiwa ni pamoja na mauaji ya albino.
Nadhani kama nimekuelewa vema maudhui makuubwa katika maelezo yako ni kuwa chanzo cha hayo yote imebase sana katika uchumi wa wananchi na jinsi uchumi wetu unavyoongozwa. Ni wazi kuwa katika maelezo ya Bwana Maingu serikali yetu inahusika moja kwa moja na ugawaji wa hii keki ya Taifa pamoja na mapungufu yote.
Ni kweli kuwa katika mikoa hiyo inayojihusisha sana na mauaji haya kuna malighafi nyingi sana na ni kweli usiopingika kuwa wanaosimamia ugawaji, umilikishwaji na uongozi wa malighafi hizo no serikali yetu nikiwa na maana kuwa hakuna mtu anayemiliki migodi au vyanzo vya mali hizo bila kupata kibali toka serikalini. sasa utoaji huo wa vibali ndio unaochochea among others, mauaji ya Albino.
Hali ya uchumi kwa wananchi wengi ni ya kukatisha tamaa pamoja na kuwa tumekuwa tukisikia kuwa uchumi wetu unakuwa kwa kasi hali za wananchi wetu bado haziridhishi na ndio sababu tunasema kuwna mismatch kati ya kukua kwa uchumi huu na hali ya maisha ya watu. Kwa serikali kutoa pesa za ziada kufanikisha zoezi la kura za siri ni kushughulikia dalili badala ya kujua mizizi ili kkuingoa.
Kufanikisha kura za maoni zinaweza kutusaidia kuwanasa wale wanaohusika na biashara hii lakini kamwe si kumaliza tatizo. Binnadamu kama alivyo binadamu atajaribu kutafuta mbinu yoyote kuhakikisha anakipata kile anachokihitaji.
kama pesa, utajiri unapatikana kwa kuuza viungo vya albino hata tukiwakamata wanaoua albino tunawezajikuta tunawasaidia watafute mbinu nyingine ya kupata viungo hivyo- tusijeshangaa kushuhudia albino wengi wakipotea au wakiuwawa kwa sababu za wizi au nyinginezo ambazo zitahalalisha mauaji yao, Hii ni kwa sababu tutakuwa tunashughulika na matokeo au dalili wakati mzizi ambao ni umasikini na ukosefu wa haki kiuchumi unabakia kukomaa na kurutubisha zaidi mauaji.
Tunaua maua ya mimea wakati tunazidi kuwekea mbolea na maji katika mashina ya mmea huo. nadhani bwana Mahingu ametoa measures ambazo ni za muhimu sana. Maana yake anajaribu kutupa ushauri wa kukabiliana na mizizi ya tatizo na si dalili za tatizo (deal with the root cause and not symptoms)
Festo E. Maro : Sunday, May 3, 2009
Nimefurahishwa na michngo iliyotumwa na wanataknet, hii inaonyesha kuwa ni jinsi gani mauaji ya albino ni aibu na ni kero katika jamii yetu. Maoni yaliyotumwa kama alivyosema Dora yanaelezea chanzo au nia inayowasukuma watu kuwauwa Albino pamoja na wanajamii wengine wanao onekana tofauti kidogo.
Ingawa vyanzo ni vingi lakini mimi naona lengo ni kupata pesa, iwe kupitia uongozi au biashara. Naona Dora anataka michango ya matokeo ya kura za siri za kutaja wahalifu. Mimi binafsi sijasikia kitu chochote kimefanyika. Labda bado uchunguzi wa taarifa zilizo kusanywaunaendelea.
Measures taken by the government so far are encouraging but they are not sufficient. There are others which I considered as passive and active. Appointment of a legislative member I consider it as passive and additional costs for running the parliament (which sometime lack funds to hold special committee meetings).
Albino is as any other human being, by appointing someone just by skin color it rather creates peculiarity of Albinism. I support the measures taken at local government level and to be specific at village level. Security committee have been put in place.
According to the information I heard, the committee are given total counts of albino and their houses to protect. This measure is recommendable but to avoid corruption the salary and other allowances given to the parliamentarian should be given to security committees as honorarium for the on e who will catch culprits.
This will motivate the committees to work even harder to protect the Albinos. This is just my opinion but am not trying to underestimate what has been done but trying to think different scenerios to revert the trend.
Admin : Thursday, April 30, 2009
Matukio ya mauaji ya walemavu wa ngozi, uchunaji wa ngozi na kunyofoa baadhi ya viungo vya miili ya binadamu ni mambo ya kushangaza lakini yanatarajiwa kutokea katika mfumo wa maisha tunayoishi. Kichocheo kikubwa ni ongezeko la pengo kati ya walionacho na wasionacho. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema hivi. "Endapo pengo kati ya walionacho na wasionancho litaachiwa kuongezeka, hakika mlipuko ni wa lazima" Kinachotokea sasa hivi miongoni mwa jamii yetu, ujambazi, wizi, ufisadi, mauaji ya kinyama, udandanyifu na tamaa ya watu wanaotaka kujitarisha ndiyo milipuko yenyewe. Na kwa bahati mbaya milipuko hii ina nguvu kubwa ya ushawawishi na imeteka fikra za viongozi wa ngazi zote (serikali, dini, mila na hata mtu mmoja, mmoja) kiasi cha kutufanya tushughulikie milipuko zaidi kuliko kuangalia mambo ya msingi.
Kwa hiyo tumejikuta tumevutwa na hiyo milipuko na tunatumia muda mwingi kuishughulikia badala ya kuangalia mambo a msingi. Serikali iko tayari kutoa fedha za dharura (tsh 200 milioni!) kuwezesha zoezi la kupiga kura ya kubaini wauaji wa albino, wakuu wa wilaya wanawawaya na kujikuta wanatoa amri zisizotekelezeka, viongozi wa dini wanatumia nguvu kubwa ya kukemea vitendo hivyo katika mauhubiri na kusahau kuwa tumeua misingi mikuu ya malezi katika familia. Watu mmoja mmoja au kwa makundi wanatafuta njia mbadala za kujihami na wakati mwingine wwanajichukulia madaraka mikononi. Misururu ya maandamano na kongamano ya kulaani vitendo hivi yanachukau nafasi kubwa. (watu wote wanavaa t-shirts na kofia nyeupe). Vyombo vya habari vi natimiza wajibu wake na kutufanya uwe na kiu ya kusikia ni wapi albino kauwawa, wezi wameiba na kubaka, viongozi wamekemea nk.
Hebu turejee muktadha (context) wa matukio haya kwa kifupi.
Mauaji ya vikongwe yalishamiri sana mikoa ya Shinyanga na Mwanza. Hata mauaji ya albino yana nguvu kubwa katika hiyo mikoa pamoja na Kagera na Mara. Hii ndiyo mikoa yenye utajiri mkubwa wa raslimali ya asili (madini na vito-dhahabu na almasi, samaki-sangara na sato, misitu kwa mazao ya mbao, mbuga za wanyama-serengeti nk). Lakini pia tunafahamu kuwa hii ndiyo mikoa ambayo wananchi wake ni maskini wa kupindukia (esrf mnazo takwinu mtusaidie). Maswali ya kujiuliza ni je, utajiri huu uko mikononi mwa watu gani na ni wangapi? (esrf mnazo takwimu-waambie wananchi wajue). Mfumo wa sera za uwekezaji umewaondoa wananchi wenyeji (wachimbaji madini wadogo wadogo, wavuvi wasio na mtaji, wawindaji wa vimoro) katika uzalishaji. wachache wanaomiliki hizo njia kuu za uchumi (kinyume na azimio la arusha) wanatafuta kila njia ya kuhodhi uongozi, na uzalishaji. (hebu rejea historia ya viongozi wa kisiasa katika maeneo haya) Nidhahiri basi kuwa hapa PENGO kati ya walio nacho na wasio nacho limekuwa kubwa kupindukia na kwa hakika hiyo ndiyo milipuko yenyewe!
Ninahisi kuwa kundi hili ndogo la walionacho ndiyo wanaohusika kwa njia moja au nyingine kuwatia wananchi hofu ili wasitawalike kwa kuchochea na kufadhili ujambazi, utumiaji wa madawa ya kulevya na hata imani za kishirikina. Lakini pia inawezekana ni baadhi ya wananchi wachache waliochoka na waliokata tamaa mithili ya wale waarabu wanajilipua kwa mabomu mbele ya watu wasio na hatia! Kwa hiyo mauaji ya albino na vikongwe ni staili tu na huenda ikabadilika katika muda mfupi ujao.
Nini Kifanyike?
Kwanza, tuwe macho tunapokimbizana na milipuko. Walioianzisha milipuko hii wanajua tutanasa katika mtego wao na kutumbukia huko wakati wao wananeemeka, wakati mwingine kwa kutumia harakari hizo hizo za kutaka kuwaokoa alibino. tusitafute muarobain i wa kuuzuia maujai ya alibin pekee. Udhalimu, uoenevu, unyanyasaji umepanuka sana na wananchi wengi wanateeka bila hata kusema.
Pili, wasomi na watafiti wetu watusaidie kutuongoza kurejea matokeo ya utekelezaji wa sera zetu na mifumo ya utawala, hasa kipindi hiki tunapokarubia uchanguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani. Viongozi wetu hasa ngazi ya jamii tunawapata vipi? wana sifa gani? wana umakini na uchunu wa watu kwa kiasi gani?. Asasi za kiraia zina nafasi kuba hapa.Sera setu za kuondoa umaskini zimetufikisha wapi, kule mwanza, shinyanga, mara, kagera, dar es salaam bagamoyo nk? MKUKUTA umewasaidaje haya makundu yanayouwawa? Mkukuta umeleta yaliyootarajiwa? na kama bado tufanye nini.
Ili kuwa na mjadala unaoleta tija esrf watuandalie mazingira ya kuchambua hii hali. Tupeni takwinu na lessons za tafi zenu.
Kwa niaba ya : Japhet Maingu Makongo,
Dorah Semkwiji : Tuesday, April 28, 2009
Kaka Hassan kwa kweli mchango wako una mengi ya kutukumbusha. Ni kweli kabisa tulikuwa tunaambiwa kuwa hawa ndugu zetu huwa hawafi, wanapotea tu yaani inawezekana kabisa walikuwa wanauawa bila watu wengi kujua.
nakubaliana nawe pia kuwa kama alivyosema Peter Ash wengi wetu hatuna ufahamu wa kutosha juu ya u-albino. Tungeelewa ingetusaidia sana kuondoa stigma iliyopo.
Mpaka sasa tumepata sababu kuu tatu ambazo zinaaminika kusababisha tatizo hili nazo ni kijamii kwa maana ya ushirikina (hii imekuwa ikitajwa sana ingawa ni ngumu kuihakiki kisayansi; ya pili ni kisiasa kama alivyotueleza kaka Nyanje na kiuchumi ambayo inahusiana moja kwa moja na hali ya umasikini.
Je tunasemaje kuhusu jitihada zinazochukuliwa mpaka sasa? Tumezungumzia kidogo kuhusu kura za maoni za siri, je tunaweza kufanikiwa kupitia njia hii? vipi kuhusu njia nyingine ambazo zimechukuliwa na serikali yetu na mashirika yasiyo ya kiserikali ?
Abdallah Hassan : Monday, April 27, 2009
Nakumbuka nilikuwa nasikiliza kipindi kimoja cha Sauti ya America (VoA) ambapo Peter Ash mwana harakati katika kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (albino) alitaja sababu kuu mbili zinazosababisha mauaji haya, kuwa ni matarajio ya kupata utajili na pia kukosekana kwa ufahamu kuhusu u-albino.
Cha kushangaza anasema zaidi ya nusu ya matukio ya mauaji ya albino yanawahusisha ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu. Sasa kitu cha kujiuliza ni kwamba hawa ndugu wanafanya hivyo ili kuondoa mkosi kama dada Dora anavyosema hapo juu, au ni kwa sababu ya umasikini – ilikupata kipato (kwa sababu nadhani hawa ndugu wanafanya kuwauzia wale ambao wanaamini viungo vya albino vina uwezo wa kuleta utajili) Mtakumbuka iliripotiwa Kijana mmoja alikamatwa Kigoma akiwa anampeleka mkewe kumuuza.
Kama hivi ndivyo, hivi kweli watanzania tumefikia hatua ya kuuza ndugu zetu kwa kisingizio cha umasikini? Inasikitisha kusikia walemavu wa ngozi wanakuwa na wasiwasi wanashindwa kuwaamini hata ndugu zao wa damu! Ash anasema pamoja na ndugu hata askari polisi wamekamatwa na kuhusishwa na matukio haya! Wamuamini nani? Ebutujiulize kwa hali hii hivi hawa ndugu zetu wanalala usingizi? Je wanatembea kwa amani?
Kunaimani pia kwamba huko nyuma watu waliamini kwamba walemavu wa ngozi walikuwa wakipotea. Walikuwa hawafi bali walikuwa wakitoweka tu! Hili linaweza kuhusishwa moja kwa moja na hoja za dada Dora kwamba huwenda walikuwa wakiuwawa ili kuondoa mkosi kwa usiri mkubwa! Pia japo sijaangalia takwimu vizuri, inaaminika kwamba idadi ya walemavu hawa hivi karibuni imeongezeka ukilinganisha na siku za nyuma! Hivi hili linaweza kumaanisha mauaji haya yamekuwepo siku nyingi bali yalikuwa yakifanyika kimya kimya?
Majuzi nilikuwa nasubiri ndege Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenyata - Kenya, nikiwa katika duka mmoja kijana mmoja mdogo aliyekuwa akiuza katika duka hilo aliniuliza wewe ni mtanzania? Nikamjibu kifua mbele ndio! Akaniuliza vipi haibu ya mauaji ya ma-albino imekwisha? Jeuri ikaniishia, nikanyong’onyea kabisa!
Watanzania hivi ni vipi tunaweza epuka aibu na fedhea hii? Nini kifanyike kumaliza unyama huu?
Dorah Semkwiji : Monday, April 27, 2009
Nakumbuka kuna makala moja ilitolewa na Hayati Munga Terenan katika gazeti la Jitambue. Yeye alifananisha na kisa cha mtu mmoja aliyegombana na jirani yake na kisha kumwambia ’tutaona kama utafika kesho.” Ilipofika alfajiri ya hiyo kesho, wakati jirani anaenda kujisaidia, akapigwa na kitu kizito kisogoni na kufa. Polisi walipofika kwenye eneo la tikio na kuhoji majirani, waliambiwa kuhusu maneno yale ya jirani.Polisi walikimbia kwenda kumkamata jirani yule. Walimtuhumu kuwa ndiye muuaji. Jirani alikanusha kwamba, hahusiki, lakini ilikuwa vugumu kuwashawishi polisi.Alishasema hadharani na jirani wote walikiri. Ni ushahidi upi tena unahitajiwa? Yule jirani alikaa ndani ya miaka miwili akisubiri uchunguzi zaidi ukamilike.Ilitokea kama bahati kwamba, wauaji wa mtu yule wakawa wanatamba kwenye vilabu vya pombe za kienyeji. Ndugu wa mtuhumiwa akapata habari ile, wakaenda polisi kutoa taarifa. Polisi waliwakamata watu hao wanaotamba kwa kuwafungulia mashtaka, kufuatia kukiri kwamba, wao ndio waliouwa. Wauaji hao walisema kwamba, walikuwa na uadui na marehemu na walikuwa wanatafuta namna watakavyomuua bila kufahamika. Ndipo waliposikia maapizo ya jirani, akimwambia marehemu kwamba, hangefika kesho. Hapo ndipo walipoona nafasi yao imafika kutimiza lengo lao. Huo kwao ndio uliokuwa muda muafaka. Mtuhumiwa au jirani aliachiwa huru lakini baada ya kukaa ndani kwa miaka miwili huku kila mtu akiamini kwamba, ndiye aliyemuua jirani yake.
Ndiyo ilivyo kwenye hili suala la albino. Tukikumbuka zamani enzi hizo tutakubali kuwa kulikuwa na wazazi, ndugu na jamaa wa albino ambao walikuwa wakiamini kuwa na mtoto albino katika familia ni mkosi, aibu au tatizo kubwa. Je hii dhana ikoje kwa sasa?. Kama hatuna uhakika kuwa dhana hii imekwisha au haipo tena je tunaamini kwa kiasi gani kuwa albino wote waliouawa baada ya yule wa kwanza kabisa kuuawa kwa imani za kishirikina, waliuawa kwa lengo la kuchukuliwa viungo vyao kupelekwa kwa waganga? Isijekuwa ni kama kisa hiki cha jirani.
Isije ikawa wazazi, ndugu na jamaa wa albino wanaoamini kwamba, kuwa na mtoto albino ni mkosi, walikuwa wanasuburi mazingira ambayo ni mwafaka kwao kutimiza haja yao ya kuondoa mkosi huo. Hali ya uchumi wa wengi inabana, kila mmoja anajaribu kujiuliza tatizo na kutafuta suluhu. Kuna wale wanao amini kwamba, ni sera mbovu za nchi, kuna waoamini ni kwa sababu hawakusoma, wengine ni kwa sababu hawana mtaji na wengine ni kwa sababu wana laana au wamelogwa na wengine ni kwa sababu wameoa wake wenye mikosi.
Lakini kuna wengi wanao amini kwamba, ni kutokana na kuwa na watoto au ndugu ambao wana kasoro fulani. Kumbuka ulemavu kama albino kwa wengi bado ni kitendawili. Kwa hiyo, ni rahisi kwa wazazi au ndugu kuamini kwamba, ugumu wa hali ya maisha unasababishwa na kuwepo kwa mtoto au ndugu ambaye ni albino familia. Wengine sio hali ngumu ya maisha balihuamini kwamba, albino kwenye familia husababisha mikosi ya mara kwa mara kama kuugua, ndugu kugombana, wanandoa kuachana na mengine ya aina hiyo. Hawa wote nao ni watuhumiwa wazuri, ambao huenda kwa sasa wanaishi chini ya kivuli cha kauli ya yule jirani kwamba mwenzake hatafika kesho. Albino wa kwanza alipouawa na kudaiwa kwamba, ni kwa sababu za kishirikina, ikawa ni sawa na wale wauzaji ambao walikuwa pembeni wakasikia kauli ile ya’ hutafika kesho.”
Huu pia ni mtazamo mwingine uliotolewa na mwenzetu (bahati mbaya ni marehemu kwasasa) kupitia Jitambue. Sijui tunaweza kuielezeaje hii nayo.
Dorah Semkwiji : Monday, April 27, 2009
Ninafurahishwa sana na uchambuzi unaofanywa na ndugu zetu Kibamba na Nyanje. Ni kweli kwa mtu wa kawaida anaweza asipate hii direct link kati ya siasa na mauaji ya Albino Tanzania. Kama nimemwelewa vizuri ndugu Nyanje ni kuwa siasa inachangia mauaji haya si kwa kutumia viungo hivyo moja kwa moja bali hata ile kutoonyesha nia ya kutoa suluhisho sahihi la tatizo hili. Inaonekana kuchukua sura ya kisiasa zaidi mfano uliotolewa hapo juu wa Mheshimiwa waziri mkuu, ni wazi malumbano yale ya Bungeni hayakuwa na sura ya kiutanzania bali kisiasa zaidi, nani kasema, wa chama gani na je atanufaikaje na kauli hiyo. KWao wao wanalichukulia tatizo hili kama njia ya kujipatia ujiko wa kisiasa (kwa lugha ya mtani).
kura za maoni, hivi hii tunaionaje, utaratibu huu wa kupiga kura yza maoni kwa siri unaweza kweli kutusaidia katika kufichua wahalifu hawa? Ni somo gani tulilojifunza kutokana na zile kura za maoni za kuwatambua majambazi ambazo tulishawahi kuletewa? je tulifanikiwa kuwakamata hao majambazi na kupunguza ujambazi nchini? Nini ilikuwa ni vikwazo katika utekelezaji wa hii enzi hizo na ni jinsi gani tungeweza kuitumia huku kiusahihi zaidi? Je ni kweli tulifanikiwa kipindi kile?. Swali langu mimi ni je hii ilikuwa ni njia sahihi ya kutatua tatizo la mauaji ya Albino hapa kwetu.
Kama alivyochengia ndugu Kibamba hapa tunasemaje au tuamini vipi kuwa kweli taasis zetu za ulinzi na usalama zimeshindwa kazi?
Inawezakana kabisa kuwa nyuma ya imani za kishirikina tunazoambiwa kama chanzo cha haya mauaji kuna mengine mengi ambayo yamemezwa na dhana hiyo ambayo bila kuyafumbua sidhani kama tutafanikiwa katika vita hii. Tunawezajikuta tumewafungia waganga wote vibali na leseni au hata kuwatia ndani na bado tukawatunashuhudia matatizo zaidi.
Peter Nyanje : Thursday, April 23, 2009
Kuingia kwa siasa katika hili kunaonekana moja kwa moja kupitia kwa wanasiasa kuligeuza suala hili kuwa ni mtaji wa kisiasa. Mfano rahisi, unaona jinsi 'walivyomsulubu' Pinda bungeni na 'kufurahia' baada ya kutoka humo. Silaumu kwa wao kukosoa kauli za Pinda, ambazo baadhi waliziona kuwa ni extrajudicial, lakini katika suala hilo hawakutakiwa kutanguliza siasa mbele... wangekosoa na kutoa suluhisho, lakini wao walionekana 'kufurahi; tu kwa 'kumsulubu' Pinda na si kuchangia mjadala kwa nia ya kutafuta suluhisho. kwa mba walifurahia ni rahisi kugundua kwani kabla ya kikao hiki kinachoendelea, niliwahi kusoma mahali fulani wapinzani wakijigamba kuwa watakwenda kumbana Pinda hadi alie tena!
Ukija kwenye suala la kupiga kura za kuwatambua wanajoihusisha kwenye mauaji ya albino, ule mkakati wa kuhamasisha wananchi washiriki nao ulichukua mrengo wa kisiasa kwa maana kuwa kuna tarifa kutoka baadhi ya sehemu kuwa vyama vya siasa vilifanya kampeni (za chinichini) kuzuia wafuasi wao wasishiriki.
Lakini hata serikali iliyoamua kutumia kura ya maoni kama njia muafaka, haikuwa siasa hii? Kwa sababu naamini kwua hii kura haiwezi kusaidia lolote katika vita dhidi ya mauaji ya albino. waplelezi kutoka usalama wa taifa wangeweza kuifanya kazi hii vema kuliko kura ya maoni. Interpol wametumia resources kidogo tu lakini wameshapata orodha ya washukiwa ambayo naamini itakuwa comprehensive kuliko matokeo ya kura ya maoni.
Kuhusu watu kudanganyika imekuwa rahisi kama ulivyosema moderator kutokana na desperation yao. Njia halali za kutafuta kipato ni kama zimezibwa (maana ni vigumu kupata mali kupitia hizo), watu wakiwaangalia mafisadi walivyonufaika narasilimali za nchi, lazima na wao watatafuta njia za mkato za kupata utajiri, ndio wanaangukia huko
Admin : Thursday, April 23, 2009
Usiasa unaingiaje ? Nakubaliana na Dora kwa kipande kikubwa. Siku hizi kila jambo likitokea tunalaumu siasa. Siasa ni kitu gani ? Mjadala huu ungenufaika sana na ufafanuzi wa wanaoamini siasa inachochea au kuchangia mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino. Labda kama unasema wanasiasa wanachangia kwa kuwa ni wateja wazuri wa viungo hivi kwa ajili ya kuendea mlingotini, Sumbawanga na Mkuranga. Lakini hebu tuwe wana sayansi, tutafiti nini hasa chanzo cha mauaji haya ya kinyama ?
Nina hoja moja ya nyongeza kuhusu kipato. Tunafahamu kuwa kipato cha watanzania ni duni. Sawa sipingi. Lakini kipato cha wazambia ni duni pia. Aidha kipato cha Wazimbabwe miaka miwili mitatu iliyopita mpaka leo kilikuwa ni zaidi ya duni. Lakini Zimbabwe hawaui walemavu wala hatukusikia mauaji ya kujipatia kipato. Asilani ! Kipato ni duni lakini tutafute uhusiano kati ya mauaji na kipato tuone kama ni ya moja kwa moja hivyo.
Kwa maoni yangu, kwa yote yanayotokea, tunajifunza kuwa mfumo wa kiulinzi na usalama wa raia nchini kwetu ni mbovu. Tumesikia walemavu wakiuawa, wenye vipara wakikatwa vichwa, weusi tii na weupe pee wakichunwa ngozi, viungo vikisafirishwa kona moja hadi nyingine na akina mama na kina dada wakibakwa hovyo hovyo. Tumesikia pia wimbi la watoto kubakwa na kulawitiwa, yote yakihusishwa na ushirikina. Ipo haja ya kujenga mfumo imara wa ulinzi na usalama wa raia nje ya dhana ya polisi mwenye bunduki na Gema Security mwenye kirungu. Uchunguzi umeonyesha kuwa hao kwanza ndio chanzo cha mauaji mara nyingi tu. Tumesikia Sinza, tumesikia Arusha, tumesikia mauaji ya Meneja wa Cocacola kule mbezi Beach....na mengine mengi sana. Taifa la wachache waliojifungia kwenye ngome zisiziongilika na walio wengi wakilala kwa hofu kuu mitaani si taifa endelevu na hapo ndio kinachoitwa serikali na Bunge kingetakiwa kuwajibika ili kurekebisha mfumo wa usalama wa raia. Mimi sijaelewa hata wizara ya usalama wa raia haswa ina mikakati gani katika hili. Sisemi hawana mikakati lakini nasema wamejichimbia nayo na hawamwambii mtu. Hizo ni mbinu za kiusalama za miaka ya 1860, sio leo !
Haya ndugu zangu. Mimi nipo ! DMK
On Behalf of Kibamba
Dorah Semkwiji : Thursday, April 23, 2009
Aksante sana Mr. Nyanje. Mchango wako umeeleweka vizuri sana na inakubalika kuwa wapo wanaodanganyika haraka na kwa kirahisi kiasi cah kufikia hatua ya kuweza kufanya mambo ya ajabu kama hili. Lakini tujuilize nini hasa kinapelekea watu kuwa desperate kiasi hiki cha kufanya lolote wanaloambiwa ili kupata utajiri? Je ni kweli hali ya maisha imekuwa mbaya kiasi hiki kuwa pesa haipatikani hadi mtu uresort kwenye kuitoa roho ya binadamu mwenzio? Tatizo hapa ni upatikanaji wa pesa hiyo au utafutaji wake ndio mgumu? Mazingira ya kumwezesha Mtanzania kuweza kujipatia kipato yakoje hata watu waresourt kwenye njia hii ya kinyama?
Umesema kuna namna wanasiasa wanaliendeleza suala hili namna ambayo inapelekea jitihada dhidi yake kupoteza mwelekeo, tafadhali tungependa utusaidie kufafanua hapo ni jinsi gani usiasa unaingia katika jambo hili Mr. Nyanje.
Peter Nyanje : Thursday, April 23, 2009
Mimi naamini sababu kubwa ya kuendelea kuwepo hili ni ujinga na siasa. Ujinga kwa maana kuwa wapo watu ambao wanakubali kudanganyika kirahisi kuwa viungo vya albino vinaweza kumtajirisha mtu. Kama kweli kuna watu wananunua, basi wao ndio wajinga namba moja. lakini kwa scenario nyingine, kuna uwezekano pia kuwa hali hii (kuwa viungo vya albino ni asili ya utajiri) ni kitu kilichotengenezwa to na wajanja wachache, hao wamefanikiwa kuifanya jamii nzima kuwa wajinga kwa sababu kitu chao cha kutunga kimeleta kizaazaa cha kimataifa.
Lakini wka upande mwingine, mauaji ya albino ni tatizo la kijamii. Ingawa jamii inahusisha mambo mengi, lakini jinsi suala hili linavyoendelezwa na wanasiasa, linaonekana kupoteza mwelekeo wake na hivyo kufanya hata jitihada zinazochukuliwa kukabiliana nalo, kupoteza mwelekeo vilevile.
Kama watu wa BBC walifanikiwa kumpenyeza mwandishi wao hadi kwa waganga wanaotuma watu kuleta viungo, kwa nini watu wa usalama wa taifa wameshindwa kuifanya kazi kama hiyo kiasi cha kuifanya srikali ifikirie kuwa kura ya maoni inaweza kuleta ufumbuzi?
Dorah Semkwiji : Thursday, April 23, 2009
Wapendwa wachangiaji wa TAKNET, napenda kuwashukuru kwa michango yenu katika mada mbalimbali zinazotolewa hapa TAKNET hasa katika awamu ya kwanza iliyokwisha. Ningependa kuwakaribisha tena katika awamu nyingine ili tuweze kujadili mambo mbalimbali yanayoikabili jamii yetu ya Tanzania. Kwa kuanzia mojawapo ya mada zilizoletwa katika awamu hii ya pili ni hii inayohusu tatizo lililoibuka katika nchi yetu: tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino). Hili kama tulivyokwishasikia katika vyombo mbalimbali vya habari limekuwa likiongezeka siku hadi siku. Karibuni tuweze kujadili sababu zilizopelekea kuwepo kwa tatizo hili pamoja na jitihada zifaazo ili kutatua tatizo hili. Karibuni sana.i
This topic has been closed. You can only view comments!
Tanzania Knowledge Network (TAKNET) Platform is supported by The Government of United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP) and coordinated by Economic and Social Research Foundation (ESRF).